1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine yasema imedungua kombora na droni 20 za Urusi

15 Juni 2023

Ukraine imesema hii leo kwamba vikosi vyake vimefanikiwa kudungua kombora moja na ndege zisizo na rubani 20 zenye vilipuzi zilizorushwa na Urusi

https://p.dw.com/p/4SbbR
Ukraine, Odesa | Schäden nach einem russischen Angriff
Picha: Lyashonok Nina/Ukrinform/ABACA/IMAGO

Ukraine imesema hii leo kwamba vikosi vyake vimefanikiwa kudungua kombora moja na ndege zisizo na rubani 20 zenye vilipuzi zilizorushwa na Urusi katika shambulizi jingine la majira ya usiku dhidi ya miji kadhaa ya Ukraine.

Maafisa mjini Kyiv wamesema hata hivyo makombora mengine matatu yalipiga maeneo ya viwanda kwenye mkoa wa Dnipropetrovsk  uliopo mashariki mwa Ukraine.

soma pia:Zelenskiy ataka dunia isiiuzie Urusi vifaa vya makombora

Taarifa hizo za Ukraine zimetolewa muda mfupi baada ya gavana aliyewekwa na Moscow kuongoza Rasi ya Crimea kusema vikosi vya Urusi vimedungua ndege tisa zisizo na rubani kwenye mipaka yake.

Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani Crimea, iliyonyakuliwa na Urusi mnamo mwaka 2014 yameongezeka katika wiki za karibuni wakati Ukraine inatanua operesheni yake ya kujibu mashambulizi ya Moscow.

Taifa hilo limedai kupata mafanikio fulani kwenye uwanja wa vita, licha ya Urusi kuzidisha hujuma zake za usiku zinazoilenga miji ya Ukraine.