1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yapuuzia kauli kuwa haijapata mafanikio vitani

29 Novemba 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ukraine Dmytro Kuleba amepuuzilia mbali wasiwasi kuwa jeshi la Ukraine halijapiga hatua katika operesheni yake ya kuyajibu mashambulizi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4Zaxe
Diplomasia | Waziri wa Mambo ya Nje Ukraine Dmytro Kuleba na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg
Waziri wa Mambo ya Nje Ukraine Dmytro Kuleba akiwa na Katibu Mkuu wa NATO Jens StoltenbergPicha: Virginia Mayo/AP Photo/picture alliance

Akizungumza leo mjini Brussels ambako anahudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa Jumuiya ya Kujihami - NATO, Kuleba amesema hakuna mkwamo wowote.

Kuleba amesema alitamani kuweka wazi kile ambacho mawaziri wenzake wamejadili katika mkutano, lakini amewahakikishia waandishi wa habari kwamba hakuna mkwamo wa kijeshi na njia iko wazi ya msaada zaidi kwa Ukraine.

Soma pia:Mawaziri wa NATO wakutana na kuahidi mshikamano na Ukraine

Kuleba anakutana na mawaziri wenzake wa NATO kujadili hali ilivyo katika uwanja wa vita na uungwaji mkono wa Kyiv kutoka nchi za Magharibi.

Kwa mara nyingine ametoa wito kwa wanachama wa NATO kuongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa silaha na vifaa vingine vya kijeshi ili kuiunga mkono Ukraine.