1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yapongeza mafanikio ya kwanza mjini Bakhmut

15 Mei 2023

Ukraine imeonesha kuridhishwa na hatua iliyochukuliwa na jeshi lake katika uwanja wa mapambano katika mji wa Bakhmut, eneo lililoshuhudia mapigano makali na ya muda mrefu tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4RMJj
Ukraine | Ukrainischer Panzer bei Bachmut
Picha: Libkos/AP PhotoZ/picture alliance

Kamanda wa jeshi la ardhini Oleksandr Syrskyi ameielezea hatua ya jeshi la Ukraine kuelekea katika mji wa Bakhmut kuwa ni mafanikio ya kwanza katika dhamira yao ya kuudhibiti mji huo.

Urusi: Ukraine imetumia makombora ya Uingereza kuwalenga raia

Kauli ya kamanda hiyo inakuja baada ya mkuu wa kundi la mamluki la Wagner la Urusi, ambalo linaongoza mashambulizi ya Urusi katika mji wa Bakhmut, kudai kuwa wanajeshi wa Urusi walikuwa wanaukimbia mji huo.

Mji huo wa eneo la mashariki na wenye viwanda awali ulikuwa na wakaazi 700,000 umeharibiwa vibaya kufuatia miezi kadhaa ya mapigano.