1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yapokea miili 250 ya wanajeshi wake waliokufa vitani

2 Agosti 2024

Mamlaka za Ukraine zinasema zimekabidhiwa na Urusi miili ya wanajeshi 250 wa Ukraine waliouawa wakati wa mapigano katika eneo linalopiganiwa mno la mashariki mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4j2vf
Jeshi la Urusi likifyatua roketi aina ya BM-21 Grad kwa uelekeo wa kuelekea Avdiivka.
Jeshi la Urusi likifyatua roketi aina ya BM-21 Grad kwa uelekeo wa kuelekea Avdiivka.Picha: Stanislav Krasilnikov/SNA/IMAGO

Makao makuu ya shirika la kuratibu matibabu ya wafungwa wa vita nchini Ukraine imesema wanajeshi hao waliuawa kwenye miji ya Bakhmut, Marinka, Avdiivka, Mariupol na kwengineko katika eneo la Donetsk lililo chini ya udhibiti wa Urusi. Katika taarifa yake, shirika hilo limesema usafirishwaji wa miili hiyo umefanywa kwa usaidizi wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu. Miili hiyo itakabidhiwa kwa familia zao kwa ajili ya mazishi baada ya kutambuliwa. Haikubainika iwapo upande wa Urusi pia ulipokea miili ya wanajeshi wake.