1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yaomba mifumo zaidi ya ulinzi wa anga kwa washirika

2 Machi 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ameyahimiza mataifa ya Magharibi hii leo kuipatia nchi yake mifumo zaidi ya ulinzi wa anga, baada ya watu wasiopungua sita kuuawa katika mashambulizi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4d6cb
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Adnan Beci/AFP/Getty Images

Mashambulizi hayo ya usiku yaliua watu wanne katika mji wa kusini wa Odesa, akiwemo mtoto wa miaka mitatu, huku shambulizi la makombora likiuwa mtu mmoja katika mkoa wa Kharkiv karibu na mpaka wa Urusi na mwingine katika mkoa wa kusini wa Kherson.

Hivi sasa Ukraine inapambana kujilinda katika vita hivyo vilivyodumu kwa zaidi ya miaka miwili, baada ya kukwama kwa msaada wa dola bilioni 60 kutoka Marekani kutokana na kukosekana kwa muafaka bungeni.

Soma pia:Shambulio la droni la Urusi lauwa watu wawili Ukraine

Urusi imefanikiwa kutwaa maeneo kadhaa hivi karibuni, baada ya jeshi la Ukraine kujitoa katika maeneo hayo.