1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yaitaka Mongolia kumkamata Rais Putin

30 Agosti 2024

Ukraine imeitolea wito Mongolia kumkamata Rais Vladimir Putin wa Urusi atakapozuru taifa hilo, ambalo ni mwanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, iliyotoa waranti wa kumkamata Putin.

https://p.dw.com/p/4k7JX
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Sputnik/Gavriil Grigorov/Pool via REUTERS

Putin anatarajiwa kwenda Mongolia wiki ijayo. 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ukraine imesema taifa hilo linatumaini kwamba serikali ya Mongolia inatambua ukweli kwamba Valdimir Putin ni muhalifu wa kivita na kuitolea mwito mamlaka kutekeleza waranti huo wa kimataifa.

Ikulu ya Kremlin kwa upande wake imesema haina wasiwasi kwamba kiongozi wake atakamatwa na Mongolia. 

Soma pia:Mawaziri wa EU wajadili mafunzo ya wanajeshi wa Ukraine

Msemaji wake, Dmitry Peskov amesema wamekuwa na mazungumzo mazuri na marafiki zao Mongolia na kila kitu kuhusu ziara hiyo kimeandaliwa kwa umakini mkubwa.