1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa EU wajadili mafunzo ya wanajeshi wa Ukraine

30 Agosti 2024

Mawaziri wa Ulinzi wa Umoja wa Ulaya wako Brussles hii leo kujadiliana juu ya operesheni inayoendelea ya umoja huo ya kuwafundisha wanajeshi wa Ukraine kuitetea nchi yao dhidi ya uvamizi wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4k6VU
Brussel, Ubelgiji | Mawaziri wa EU wakiwa katika mkutano
Mawaziri wa Ulinzi wa Umoja wa Ulaya wakiwa katika mkutanoPicha: Francois Lenoir/European Union

Mawaziri hao pia watajadiliana mpango wa kuzihamishia operesheni hizo za mafunzo ndani ya Ukraine, tofauti na Poland na Ujerumani ambako mafunzo hayo yanafanyika kwa sasa.

Ufaransa na Lithuania zimeashiria kuunga mkono hatua hiyo, licha ya wasiwasi uliooneshwa na Ujerumani na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya.

Soma pia:Jeshi la Israel lawaua 'magaidi tisa' wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi

Hakutarajiwi kufanyika maamuzi yoyote rasmi kwenye mkutano huu usio rasmi, ambao ulitarajiwa kufanyika Budapest, Hungary, lakini badala yake ulihamishiwa Brussels, kama njia ya kumsusia Rais Viktor Orban kutokana na mkutano wake na Rais Vladimir Putin wa Urusi.