1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Miji kadhaa ya Urusi yashambuliwa na Ukraine

17 Machi 2024

Mamlaka nchini Urusi zimesema Ukraine imeendesha jumla ya mashambulizi 35 ya droni na kuulenga mji mkuu Moscow na miji mingine.

https://p.dw.com/p/4dohB
Ukraine yafanya mashambulizi makubwa Belgorod
Watu wakishuhudia uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Ukraine katika mkoa wa mpakani wa Urusi wa Belgorod:16.03.2024Picha: AFP

Mashambulizi hayo ya Ukraine yamekilenga pia kiwanda cha kusafisha mafuta na kusababisha matatizo ya kukatika kwa umeme katika maeneo ya mpakani. Watu 7 wameripotiwa kuuawa katika mji wa Ukraine unaodhibitiwa na Urusi wa Kharkiv.

Gavana wa mkoa wa Belgorod Vyacheslav Gladkov amesema msichana wa miaka 16 ameuawa baada ya nyumba yake kushambuliwa na kombora kutoka Ukraine. Leo ikiwa ni siku ya mwisho ya upigaji kura nchini Urusi, Kremlin inaishutumu Kiev kujaribu kuhujumu mchakato wa uchaguzi.

Soma pia: Urusi inafanya uchaguzi katikati ya vita na Ukraine

Jeshi la Ukraine limetangaza kuwa mashambulizi ya anga ya Urusi yameharibu miundombinu ya viwanda vya kilimo katika bandari ya Odesa, huku Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu akilimuru hii leo jeshi la wanamaji kuimarisha ulinzi katika Bahari Nyeusi.