1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yadai kuikomboa wilaya muhimu ya mji wa Bakhmut

18 Septemba 2023

Ukraine imedai hapo jana kuwa vikosi vyake vimeukomboa mji mdogo wa Klishchiivka, ulio eneo la mstari wa mbele katika uwanja wa mapambano huko kwenye mji wa Bakhmut.

https://p.dw.com/p/4WS5e
Wanajeshi wa Ukraine
Wanajeshi wa Ukraine Picha: Ukrainian Presidential Chief of Staff Andriy Yermak/AFP

Kamanda wa vikosi vya ardhini vya jeshi la Urusi, Oleksandr Syrsky, ndiyo alitangaza habari hizo kupitia mitandao ya kijamii.

Muda mfupi baadaye rais Volodomyr Zelensky aliwasifu wanajeshi wanaopigana kuwania mji wa Bakhmut na kuwapongeza mahsusi wale waliofanikiwa kulichukua eneo la Klishchiivka.

Ushindi kwenye uwanja wa vita ni muhimu hivi sasa kwa Ukraine katika wakati kiongozi wake anajitayarisha kwa ziara ya pili nchini Marekani tangu Urusi ilipoivamia nchini hiyo.

Zelensky ataitembelea Washington baadaye wiki hii kwa lengo la kuomba msaada zaidi wa kijeshi kwa taifa lake kuendelea kupambana na Urusi.

Washirika wake wanaonesha kuvunjwa moyo na mwendo wa polepole wa operesheni ya Ukraine iliyozinduliwa mwezi Juni kwa dhumuni la kurejesha maeneo yote yaliyokamatwa na Moscow.