1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yaapa kulipa kisasi kwa shambulizi baya la Odesa

23 Julai 2023

Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky ameapa kulipiza kisasi kwa shambulio baya la Urusi ambalo limesababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine 22.

https://p.dw.com/p/4UHlt
Zelensky, Ukraine
Rais Volodmyr Zelensky wa UkrainePicha: Pool Philip Reynaers/belga/dpa/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky ameapa kulipiza kisasi kwa shambulio baya la Urusi ambalo limesababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine 22. Usiku wa kuamkia leo, Urusi imeushambulia mji wa bandari wa Odesa kwa makombora takribani 19 na kuharibu Kanisa kuu la Orthodox. Kanisa hilo limeorodheshwa katika turathi za dunia za Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO.

Katika taarifa yake, Moscow imesema imefanikiwa kuyalenga maeneo yote kwenye shambulio la Odessa, ikidai maeneo hayo yanatumiwa kuandaa vitendo vya kigaidi dhidi yake. Mashambulizi yameongezeka tangu Urusi ilipojiondoa katika makubaliano muhimu ambayo yaliruhusu usafirishaji salama wa nafaka za Ukraine, na kumaliza kabisa makubaliano hayo yaliyotiwa saini mwezi Julai mwaka jana kati ya Urusi, Ukraine, Uturuki na Umoja wa Mataifa. Odesa imeshambuliwa mara kwa mara tangu uvamizi uanze.