1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine waadhimisha mwaka mmoja wa ukombozi Bucha

1 Aprili 2023

Ukraine imeadhimisha ukombozi wa mji wa Bucha kwa wito wa haki baada ya uvamizi wa Urusi uliosababisha vifo vya mamia ya raia na kuufanya mji huo kuwa kitovu cha ukatili wa vita.

https://p.dw.com/p/4PaGL
Ukraine Butscha | Gedenkveranstaltung zum ersten Jahrestag der Befreiung der Stadt
Picha: Mstyslav Chernov/AP/Picture alliance

Wakati wa hafla ya maadhimisho hayo mjini Bucha, Rais Volodymyr Zelensky amesema kuwa hawataruhusu kusahaulika kwa matukio hayo na kuahidi kuwaadhibu waliofanya maasi hayo, huku akiongeza kuwa katika barabara za Bucha, dunia imeshuhudia uovu wa Urusi.

Rais wa Moldova na mawaziri wakuu wa Croatia na Slovakia pia walihudhuria maadhimisho hayo.

Soma zaidi: Ukraine: Hatutaisamehe Urusi kwa mauaji ya Bucha

Jina la Bucha linaibua ukatili wa jeshi la Urusi tangu uvamizi wake kamili nchini Ukraine mwezi Februari 2022.

Vikosi vya Ukraine vilivyoukomboa mji huo, vilikuta miili ya wanaume, wanawake na watoto katika barabara, majumbani na makaburi ya halaiki, baadhi ikionesha dalili za mateso.