1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUkraine

Ukraine, UN zataka kurefushwa mpango wa kusafirisha nafaka

8 Machi 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wametoa wito wa kurefushwa kwa mpango uliofikiwa na Moscow ambao umeruhusu Kyiv kusafirisha nafaka kupitia bandari za Bahari Nyeusi.

https://p.dw.com/p/4OPGL
Türkei I Getreidefrachter  auf Durchfahrt durch Bosporus
Picha: Yasin Akgul/AFP/Getty Images

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wametoa wito wa kurefushwa kwa mpango uliofikiwa na Moscow ambao umeruhusu Kyiv kusafirisha nafaka kupitia bandari za Bahari Nyeusi wakati wa uvamizi wa Urusi. Zelensky amesema baada ya mazungumzo na Guterres mjini Kyiv kuwa Mpango wa kusafirishwa Nafaka kupitia Bahari Nyeusi ni muhimu kwa ulimwengu, naye Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa akasisitiza umuhimu wa makubaliano hayo kwa upatikanaji wa chakula ulimwenguni na kwa bei za chakula.

Muafaka huo wa siku 120 uliofikiwa chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa na Uturuki Julai mwaka jana na kurefushwa Novemba, utarefushwa tena Machi 18 kama hakuna upande utakaopinga.