1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine kupokea bilioni dola 1.5 kusaidia kujijenga upya

30 Juni 2023

Waziri Mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal amesema Ukraine itapata kitita cha dola bilioni 1.5 kutoka kwa Benki ya Dunia ili kuisaidia nchi hiyo inayokabiliwa na uvamizi wa Urusi, kujijenga upya.

https://p.dw.com/p/4TGt3
Ukraine, Kiew | Selenskyj trifft Vertreter der Weltbank
Picha: The Presidential Office of Ukraine

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Telegram, Waziri Shmyhal amesema fedha hizo zitatolewa kwa dhamana ya serikali ya Japan na zitasaidia kuboresha mifumo ya kijamii na maendeleo ya kiuchumi.

Ukraine inategemea msaada wa kifedha kutoka kwa washirika wake wa kigeni ili kuweza kufidia nakisi ya bajeti yake. Jana, bodi ya Shirika la Fedha la Kimataifa ilikamilisha mkakati wa mkopo na hivyo kuiruhusu Kyiv kupewa mara moja dola milioni 890 ili kusaidia bajeti yake.

Ukraine inaendelea na ujenzi upya wa shule, hospitali, barabara na madaraja na kufanya ukarabati katika sekta ya nishati licha ya kuendelea mapigano kusini na mashariki mwa nchi hiyo.