1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukosefu wa ajira wapanda kwa 4% Uingereza

11 Julai 2023

Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Uingereza kimeongezeka hadi asilimia nne katika muda wa miezi mitatu kuelekea mwishoni mwa mwezi Mei.

https://p.dw.com/p/4Tjzu
Großbritannien | Rishi Sunak
Picha: Kin Cheung/REUTERS

Ukosefu huo wa ajira unatokea wakati Uingereza inakabiliwa na mfumuko wa bei za bidhaa. 

Ofisi ya Takwimu ya nchi hiyo (ONS) imesema kiwango cha ukosefu wa ajira kimeongezeka kutoka 3.8% katika miezi mitatu ya kuelekea mwisho wa mwezi Aprili.

Licha ya kiwango hicho kuongezeka, Waziri wa Fedha Jeremy Hunt amesema soko la ajira la Uingereza liko imara na kwamba ukosefu wa huo ajira uko chini tofauti na miaka ya awali.

Ofisi ya ONS imeeleza kuwa mishahara bila ya kujumuisha marupurupu imeongezeka katika viwango vya kuvunja rekodi. 

Mfumuko wa bei Uingereza umepungua katika miezi ya hivi karibuni, japo viwango bado vinakaribia asilimia tisa.