1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Gaza yakabiliwa na ukosefu wa mtandao wa intaneti

17 Novemba 2023

Ukanda wa Gaza unakabiliwa na ukosefu wa mtandao wa intaneti na mawasiliano ya simu tangu kutokana na kupungua kwa akiba ya mafuta

https://p.dw.com/p/4YzLF
Makazi ya muda ya Wapalestina nje ya hospitali ya Al Shifa mnamo Novemba 12, 2023
Makazi ya muda ya Wapalestina nje ya hospitali ya Al ShifaPicha: Ahmed El Mokhallalati/REUTERS

Hali hiyo imefanya kuwepo wasiwasi kwamba ukosefu wa huduma ya mawasiliano unaweza kuwa wa muda mrefu tofauti na ule uliotokea wiki chache zilizopita. Hitilafu hiyo ya mawasiliano kwa jumla imewaathiri karibu wakaazi wote milioni 2.3 wa Ukanda wa Gaza.

Hawawezi kuwasiliana ndani ya ukanda huo wale nje ya mipaka yake. Hali hiyo inatishia kutatiza juhudi za utoaji msaada wa kiutu hasa katika wakati hujuma za jeshi la Israel zinaendelea.

Jeshi la Israel laashiria kufanya mashambulizi Kusini mwa Gaza

Jeshi hilo limeaashiria litaelekeza mashambulizi yake eneo la kusini ambako iliamuru wakaazi wa Gaza kuhamia kutafuta hifadhi kutoka maeneo ya kaskazini.

Limesema baada ya operesheni kubwa kwenye hospitali ya Al-Shifa na mapambano ya wiki tano kaskazini mwa Gaza, sasa limechukua udhibiti kwa sehemu kubwa ya eneo hilo.