1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArmenia

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wawasili Nagorno-Karabakh

1 Oktoba 2023

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa umewasili leo kwenye jimbo la Nagorno-Karabakh baada ya karibu jamii yote ya wakaazi wenye asili ya Armenia kulikimbia tangu Azerbajain ilipochukua udhibiti kamili wa eneo hilo wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4X15f
Armenien Goris | Flüchtlinge aus Bergkarabach
Makumi kwa maelfu ya wakaazi wenye asili ya Armenia wameukimbia mkoa wa Nagorno-Karabakh Picha: Vasily Krestyaninov/AP Photo/picture alliance

Taarifa ya ofisi ya rais wa Azerbaijan imesema ujumbe huo umefika jimboni humo tangu majira ya asubuhi kwa dhumuni la kutathmini mahitaji ya kiutu na kile kinachoendelea kwenye eneo hilo.

Inakadiriwa hadi sasa wakaazi karibu wote wenye asili ya Armenia wamelikimbia jimbo la Karabakh kuepuka kile wanasema kuwa wasiwasi wa Azerbaijan kulipa kisasi baada ya kulidhibiti.

Jimbo hilo ambalo kihistoria ni sehemu ya Azerbaijan lilikuwa nyumbani kwa jamii kubwa ya Waarmenia walioendesha vuguvugu la kujitenga kwa dhamira ya kujiunga na taifa lao la asili la Armenia. 

Mzozo wa kuwania jimbo hilo ulidumu kwa miaka 30 hadi mnamo wiki iliyopita pale wapiganaji wa Kiarmenia walipoweka chini silaha na kuruhusu Azerbaijan kuchukua udhibiti wa eneo lote la Nagorno Karabakh.