1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa EAC nchini DRC warefushiwa muda hadi Septemba

1 Juni 2023

Ujumbe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa kupambana na ghasia za makundi ya waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umeongezewa muda hadi mwezi Septemba.

https://p.dw.com/p/4S39J
Konflikt im Kongo
Picha: Alexis Huguet/AFP

Hilo limethibitishwa na msemaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya mkutano wa kilele uliofanyika jana mjini Bujumbura, Burundi.

Waziri wa ulinzi wa Kongo, Jean Pierre Bemba pia amethibitisha kurefushwa huko kwa muda wa ujumbe huo ujulikanao kama EACRF, ambao uliundwa na wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Aprili mwaka uliopita.

Hatma ya ujumbe huo ilikumbwa na sintofahamu mwezi Machi , baada ya kuibuka tofauti kati ya viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu majukumu yake.