1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yazidi kushinikizwa kuisaidia Ukraine

20 Januari 2023

Ujerumani inakabiliwa na shinikizo kubwa linaloongezeka la kuitaka ipeleke vifaru vya kivita chapa Leopard nambari 2 nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4MTTf
Deutschland Kampfpanzer vom Typ Leopard 1
Picha: Tobias Kleinschmidt/dpa/picture alliance

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na viongozi wengine wameikosoa serikali ya Ujerumani kwa kujizuia kuipatia silaha nzitonzito za ziada Ukraine. Hii leo serikali ya Ujerumani na waziri wake  mpya wa ulinzi Boris Pistorius watakabiliana na mtihani wao mkubwa wa kwanza katika mkutano na maafisa wa ngazi za juu wa Marekani.Akizungumzia yatakayojadiliwa leo waziri wa ulinzi wa Ujerumani amesisitiza Marekani ni mshirika muhimu wa Ujerumani. Pistorius atakutana na waziri mwenzake wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin katika kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ramstein hapa Ujerumani kujadili suala la kuipelekea silaha zaidi Ukraine. Pistorius jana aliweka wazi kwamba nchi yake itachukua hatua kwa ushirikiano na Marekani. Marekani inaiunga mkono Ujerumani.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW