1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatafakari maombi wa uhamiaji nje ya Ulaya

29 Aprili 2023

Ujerumani inatafakari kushughulikia maombi ya uhamiaji nje ya mipaka ya bara la Ulaya

https://p.dw.com/p/4Qi4b
Flüchtlinge Deutschland 2015
Picha: Markus Schreiber/picture alliance/AP/dpa

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Nancy Faeser ameliambia gazeti la kila jumapili la hapa Ujerumani "Allgemeine Sonntagszeitung" kwamba serikali inatathmini iwapo taratibu za uombaji hifadhi zinaweza kufanyika nje ya matiafa ya Umoja wa Ulaya.Alisema kuwa mikataba ya uhamiaji kwa nchi hizo imepangwa kwa mujibu wa sheria na kuongeza kuwa serikali ilikuwa inaangalia ikiwa mazingira ya hali ya ulinzi  yanawezekana pia ndani ya mfumo huo.Kwa mujibu wa Shirika la Takwimu la Umoja wa Ulaya-Eurostat, maombi ya hifadhi yameongezeka nchini Ujerumani na katika eneo lote la Umoja wa UIaya. Kwa mfano mwaka 2022, watu 881,200 walituma maombi katika eneo hilo, na miongoni mwa hao 217,735 waliwasilisha ombi lao nchini Ujerumani.Manispaa nyingi za Ujerumani zinahisi kuzidiwa na idadi kubwa ya wakimbizi, na suala hilo linatarajiwa kujadiliwa katika mkutano wa Mei 10 utakaohusisha majimbo yote 16 ya Ujerumani na serikali ya shirikisho.