Ujerumani yapeleka misaada katika ukanda wa Gaza
20 Desemba 2023Katika vidio iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, mjumbe maalum wa Ujerumani kuhusu masuala ya kibinadamu katika eneo la Mashariki ya Kati Deike Potzel, ametangaza kuwa ndege ya kijeshi ya Ujerumani imepeleka mahema ili kuwasaidia wakaazi wa Gaza.
Potzel ameongeza kuwa, ndege mbili nyingine zitapeleka magodoro 10,000, vitanda 5,000 na idadi isiojulikana ya mitungi ya kuhifadhia maji.
Mjumbe huyo maalum wa Ujerumani kuhusu masuala ya kibinadamu katika eneo la Mashariki ya Kati ameeleza kuwa Ujerumani imeongeza kwa kiasi kikubwa misaada na itatoa kiasi dola milioni 220 kwa ajili ya kuyasaidia mashirika mbalimbali ya kibinadamu.
Amesema "Ujerumani inataka kusaidia watu wa Gaza," na ameapa kuwa serikali ya mjini Berlin inafuatilia kikamilifu sera zake za nje katika ngazi zote ili kupunguza mateso kwa wakaazi wa Gaza.