1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaonya dhidi ya uvumi wa kifo cha Prighozhin

24 Agosti 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ameonya juu ya uvumi kuhusiana na ajali ya ndege ambayo mamlaka zinasema miongoni mwa abiria waliokufa ni kiongozi wa kundi la Wagner, Yevgeny Prighozhin.

https://p.dw.com/p/4VXKK
Berlin PK Außenministerin Annalena Baerbock
Picha: Bernd Elmenthaler/IMAGO

Amekiambia kituo cha radio cha Ujerumani cha Deutschlandfunk kwamba hakuna hitimisho la haraka linaloweza kutolewa ingawa amesema kisa hicho kinadhihirisha kwamba mfumo, au mamlaka ama udikteta uliojengwa kwa misingi ya vurugu pia utakumbwa na vurugu za ndani.

Ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria sana na wafanyakazi watatu ilianguka karibu kilomita 300 kaskazini magharibi mwa Moscow.

Bado kuna sintofahamu kubwa juu ya taarifa za kifo cha mkosoaji mkubwa wa masuala ya ulinzi nchini Urusi, huku mataifa ya magharibi yakionyesha mashaka ya wazi kuhusiana na taarifa hizo.