1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yalipiga marufuku kundi la Hammerskins

19 Septemba 2023

Serikali ya Ujerumani imelipiga marufuku kundi la Hammerskins la Wanazi Mamboleo lenye makaazi yake nchini Marekani, ambalo ni mashuhuri kwa kufanya matamasha ya itikadi kali ya watu weupe.

https://p.dw.com/p/4WXq7
Deutschland | Razzia gegen Neonazi-Gruppe in Berlin
Picha: Dominik Totaro/dpa/picture alliance

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani iliyotolewa siku ya Jumanne (Septemba 19) ilieleza kuwa kundi hilo lenye takribani wafuasi 130 linalenga kueneza siasa kali za mrengo wa kulia na kibaguzi kwa kuzingatia itikadi ya Unazi Mamboleo. 

Polisi walivamia nyumba 28 za wanachama wa kundi hilo kwenye majimbo kadhaa ya Ujerumani mapema siku ya Jumanne. 

Soma: Kushamiri kwa itikali kali za kulia huenda kukazuwia uhamiaji wafanyakazi wenye ujuzi

Baadhi ya matawi ya kundi hilo na jengine liitwalo Crew 38, ambalo pia lina mafungamano na Hammerskins, pia yamepigwa marufuku. 

Kwa mujibu wa wizara hiyo, kundi hilo lililoanzishwa mwaka 1988 limekuwa na mchango mkubwa katika kuenezea itikadi kali za mrengo wa kulia barani Ulaya "ambazo ni kitisho kikubwa kwa demokrasia ya Ujerumani."