1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa maendeleo wa Ujerumani ziarani Afrika

15 Agosti 2019

Waziri wa maendeleo wa Ujermani Gerd Müller amezuru eneo la Afrika mashariki na kati, kusaidia uwekezaji, mapambano dhidi ya Ebola, pamoja na kuimarisha utunzaji wa mazingira na kukukabiliana na mabadiliko ya tabiachi.

https://p.dw.com/p/3NyTk
Gerd Müller Bundesminister für wirtschaftliche Zusammenarbeit und Entwicklung
Picha: picture-alliance/dpa/J-U Koch

Wakati wa ziara yake nchini Rwanda, waziri huyo wa maendeleo wa Ujerumani Gerd Müller ameahidi msada mpya wa Ujerumani wenye thamani ya karibu euro milioni 25 kwa taifa hilo la afrika ili kukuza elimu na uhifadhi wa mazingira.

Serikali ya Ujerumani inatoa euro milioni 9.5 kwa ajili ya mkakati mpya, wa mafunzo na ajira, ambao utaanza mwezi ujao katika mji mkuu wa Rwanda Kigali.

"Kwa sababu ni muhimu kukipa mafunzo ya ufundi kizazi cha vijana. Kutoa mafunzo kwa vijana - na kuunda nafasi za ajira baadae, alisema waziri Müller.

Nafasi 4500 za mafunzo pamoja na 2200 za ajira zimepangwa. Katika mwaka ujao, kiwango sawa cha msaada kimepangwa kutolewa na Ujerumani. Zaidi ya hayo, waziri Müller ameahidi kiasi cha euro milioni 15 kwa ajili ya miradi ya uhifadhi mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Ruanda Bundesentwicklungsminister Gerd Müller in Kigali
Waziri Müller akitembelea kituo cha IPRC mjini Kigali, 11.08.2016. Ujerumani imekuwa mshirika muhimu wa maendeleo wa Rwanda kwa miaka kadhaa sasa.Picha: picture-alliance/dpa/U. Grabowsky

Afrika kuionesha Ulaya inavyofanyika

Kupitia miradi hiyo, majiko ya kuni na mkaa ambayo ndiyo yanatumika kwa ajili ya kupikia katika maeneo mengi ya Rwanda, yanapagwa kuondolewa, na nafasi yake kuchukuliwa na majiko ya nguvu za jua kwa mfano. Mradi wa Mji wa Kijani wa Kigali, unalenga kukuza aina mpya za nyumba na usafiri unaozingatia utunzaji wa mazingira.

"Mjini Kigali, sisi - wizara ya ushirikiano wa maendeleo ya Ujerumani na washirika wa Rwanda - tunalenga kujenga mji wa mfano, kanda ya mfano tuseme. Afrika inaionyesha Ulaya namna inavyofanyika."

Waziri wa maedeleo wa Ujerumani ameisifu Rwanda kama nchi ya mfano na anataka kuisadia kuvutia uwekezaji zaidi.

Pendekezo lake: Wakati mataifa ya yaliomo kwenye mkakati wa maendeleo ya kimataifa wa Compact Afrika yatakapokutana mjini Berlin mwezi Septemba, kuweze kufanyika mkutano maaluumu wa kuvutia uwekezaji nchini Rwanda.


Baada ya ziara hiyo nchini Rwanda, Waziri Müller, ambaye asubuhi alikuwa mjini Nairobi, ameendeleka katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.


Chanzo: DW