1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin, Paris kuimarisha ulinzi, usalama na uchumi wa Ulaya

29 Mei 2024

Ujerumani na Ufaransa zinapanga kuimarisha ulinzi, usalama na uchumi barani Ulaya. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa baada ya kumalizika kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

https://p.dw.com/p/4gOcV
Mkutano wa viongozi wa Ujerumani na Ufaransa katika kasri la Meseberg
Rais Macron na Kansela Scholz wameahidi kuimarisha uchumi, usalama na ulinzi barani UlayaPicha: Annegret Hilse/REUTERS

Ujerumani na Ufaransa zinapanga kuimarisha ulinzi, usalama na uchumi barani Ulaya. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa baada ya kumalizika kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mashauriano ya serikali karibu na mji mkuu Berlin.

Baraza la Ulinzi na Usalama la Ufaransa na Ujerumani limesema kutokana na kubadilika kwa hali ya usalama Ulaya, Ufaransa na Ujerumani zinapanga kuimarisha uwezo wa ulinzi barani humo. Limesema Umoja wa UIaya lazima uwe kinara wa kweli wa siasa za kikanda na mlinzi wa usalama anayeweza kushughulikia changamoto za sasa za usalama.

Soma pia: Macron aonya dhidi ya kuenea siasa za misimamo mikali Ulaya

Kuhusu Ukraine, Kansela Scholz amesema Ujerumani na Ufaransa zinayataka mataifa yaliyostawi kiviwanda Ulaya kutoa msaada wa mabilioni kwa nchi hiyo iliyoko vitani na Urusi.

Amesema uwezekano wa kutumia faida za mali za Urusi zinazoshikiliwa Ulaya unachunguzwa. Mapema jana kabla ya kukutana na Kansela Scholz katika Kasri la Meseberg karibu na Berlin, Macron alitunukiwa tuzo ya kimataifa ya amani ya Westphalia mjini Münster.