1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Ujerumani kuipa Ukraine magari 40 ya kivita chapa ya Marder

6 Januari 2023

Ujerumani inapanga kuikabidhi Ukraine magari ya kijeshi chapa ya Marder, katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4LpcZ
Deutschland liefert Marder-Panzer und Patriot-System an Ukraine
Picha: BeckerBredel/IMAGO

Hayo yameelezwa leo na Msemaji wa Serikali ya Ujerumani Steffen Hebestreit. Amesema kuwa magari hayo ya kivita yapatayo 40 aina Marder yatapelekwa Ukraine.

Hebestreit amesema Marekani pia itawapatia mafunzo wanajeshi wa Ukraine kuhusu matumizi ya vifaru aina ya Bradley. Ujerumani na Marekani pia zimeahidi kuipatia Ukraine mitambo ya kurushia makombora aina ya Patriot.

Wakati huo huo, miji kadhaa mashariki mwa Ukraine imeshambuliwa leo katika majibizano ya makombora, licha ya kiongozi wa Urusi Vladmir Putin kuviamuru vikosi vyake kusitisha mapigano kwa muda wa saa 36. Urusi imesema inaheshimu usitishaji mapigano na imeishutumu Ukraine kwa kufanya mashambulizi hayo.