1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

NATO yaikumbusha Ujerumani kuongeza mchango wa ulinzi

17 Septemba 2023

Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg ameiongezea shinikizo Ujerumani akiitaka kuongeza mchango wake wa ulinzi katikati ya vita vya Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4WRT1
Katibu mkuu wa Jumuiya ya kujihami, NATO Jens Stoltenberg alipokuwa kwenye mkutano wa masuala ya ulinzi huko Vilnius, Lithuania Julai 10, 2023
Katibu mkuu wa Jumuiya ya kujihami, NATO Jens Stoltenberg alipokuwa kwenye mkutano wa masuala ya ulinzi huko Vilnius, Lithuania Julai 10, 2023Picha: PETRAS MALUKAS/AFP

Kwenye mahojiano na shirika la habari la Ujerumani Funke, katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amekumbushia enzi ya Vita Baridi wakati makansela Konrad Adenauer na Willy Brandt walipochangia asilimia tatu hadi nne ya pato la taifa kwenye bajeti ya ulinzi.

Amesisitiza kama hilo liliwezekana wakati huo, ni lazima lifanyike tena sasa.

Muda mfupi baada ya Urusi kuivamia Ukraine, kansela wa Ujerumani Olaf Scholz aliahidi yuro bilioni 100 ya bajeti ya mwaka 2022 ya matumizi ya kijeshi na pia aliahidi kufikisha asilimia mbili ya pato la ndani la Taifa kwenye matumizi ya ulinzi ya NATO.