1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani haikutikiswa na matukio ya 2023 - Scholz

31 Desemba 2023

Katika hotuba yake ya Mwaka Mpya, Kansela Olaf Scholz amesema Ujerumani italazimika kubadilika mbele ya uso wa ulimwengu "usio na utulivu," lakini alionesha uhakika kuwa nchi hiyo "itayashinda hayo."

https://p.dw.com/p/4ajrk
EMBARGO BEACHTEN - Deutschland Olaf Scholz Neujahrsansprache 2023/2024
Picha: Markus Schreiber/AP/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kwenye ujumbe wake wa mwaka mpya amekiri juu ya mazingira tete ya kiulimwengu, ingawa kwa upande mwingine akionyesha imani yake kwamba Ujerumani itashinda.

Scholz amezungumzia mateso makali, umwagikaji mkubwa wa damu na kukiri kwamba ulimwengu kwa sasa umekuwa mahali pagumu, hii ikiwa ni kulingana na matamshi yaliyoko kwenye hotuba yake iliyotolewa na ofisi yake kabla ya kurushwa kwenye mkesha wa mwaka mpya.

Kiongozi huyo wa Ujerumani hata hivyo ameelezea matumaini huku akiviangazia vikwazo vya ndani na kimataifa ambavyo nchi hiyo ilivishinda kwa 2023.

Kimataifa, Scholz amezungumzia uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2024, na hasa wa Marekani, Uingereza, India na Bunge la Ulaya, huku akirejea umuhimu wa uchaguzi huo na hasa wa Marekani, katikati ya vita vinavyoongezeka nchini Ukraine na Mashariki ya Kati.