1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yadaiwa kuendesha shughuli za polisi nchini Ujerumani

15 Mei 2023

Wizara za mambo ya nje na ndani ya Ujerumani zimesema vyombo vya usalama vya Berlin vinaamini China bado inaendesha shughuli za polisi wa siri Ujerumani, licha ya Beijing kutoa hakikisho kuwa iliacha kufanya hivyo.

https://p.dw.com/p/4RN4V
Deutschland | Symbolbild Polizeieinsatz
Picha: Bjoern Trotzki/IMAGO

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani wa Ujerumani ameuambia mkutano wa waandishi habari kuwa, mamlaka za usalama zinashuku uwepo wa vituo viwili vya polisi vya China nchini Ujerumani.

Msemaji huyo amefafanua kwa, vituo hivyo vya polisi vya China havikuwepo kwenye eneo maalum bali ni vya kuhamahama na kwamba raia wa China na wasio Wachina wamekuwa wakifanya "kazi rasmi" kwa niaba ya Beijing.

Ujerumani iliitaka China mnamo mwezi Novemba kufunga vituo vyake vya polisi vilivyoko nje ya mipaka yake.

Ubalozi wa China mjini Berlin haukujibu mara moja ombi la kutoa kauli yake juu ya suala hilo.