1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yawachanja zaidi ya watu milioni ishirini

Saleh Mwanamilongo
1 Machi 2021

Uingereza imesema itaanza kutoa chanjo kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 40. Hapa nchini Ujerumani idadi ya vifo vya Covid-19 imefikia zaidi za 70 elfu.

https://p.dw.com/p/3q3Iw
Johnson & Johnson Impfstoff
Picha: Johnson & Johnson via REUTERS

Waziri wa Afya wa Uingereza, Matt Hancock amesema zaidi ya watu milioni 20 wamepatiwa alau dozi dozi ya kwanza ya chanjo.

'' Tunamatumaini makubwa kwamba chanjo ina kukinga, inakinga jamii yako na ni njia ya kutukwamua sote katika janga hili. Njia bado ni ndefu,lakini tumepiga hatua kubwa za mafanikio.''

Uingereza iko mbele ya nchi nyingine za Ulaya katika kutoa chanjo kwa wananchi wake kwa kuongeza muda wa kusubiri kati ya dozi mbili hadi miezi mitatu, ili watu zaidi wapewe chanjo haraka.

Waziri Mkuu wa Uingereza  Boris Johnson alisema hatua hiyo ni mafanikio makubwa ya kitaifa na alipongeza kazi ya wafanyakazi wa huduma ya afya wa nchi yake.

Uingereza inaidadi kubwa ya vifo vinavyotokana na Covid-19 barani Ulaya na iliathirika na kirusi kipya ambacho kinaambaukiza zaidi. Lakini katika wiki za hivi karibuni, nchi hiyo imeshuhudia kupungua kwa visa vya maambukizi ya corona.

Ujerumani ya rikodi visa vipya

Aidha, idadi ya visa vya virusi vya corona nchini Ujerumani imeongezeka kwa 4,732 hadi 2,447,068. Taasisi ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza ya Ujerumani, Robert Koch imesema idadi ya watu waliokufa imefikia 70,105 baada ya kuwepo vifo vipya 60.

Iran imerekodi vifo 60 elfu vya  covid-19 na idadadi ya mamabukizi imefikia milioni 1.6 katika nchi hiyo ambayo ni miongoni mwa nchi zilizoathirika vibaya na janga la Covid-19.

Waziri MKuu wa India, Neranda Modi akipewa chanjo dhidi ya Covid-19 jijini New Delhi.
Waziri MKuu wa India, Neranda Modi akipewa chanjo dhidi ya Covid-19 jijini New Delhi.Picha: Narendra Modi/twitter/AP Photo/picture alliance

 Kwa upande wake, India imepanua kampeni yake ya chanjo dhidi ya covid-19, mbali na wahudumu wa afya kampeni hiyo inawalenga watu wenye umri wa miaka 60 au chini ya umri huo . Miongoni mwa waliopewa chanjo hiyo ni pamoja na Waziri Mkuu wa India, Narenda Modi. India inalenga kuwapa chanjo watu milioni 300 ifikapo Agosti.

 Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema nchi hiyo itaanza kulegeza masharti yaliyowekwa kuzuia kuenea virusi vya corona, baada ya maambukizi kupungua.

Ziara ya Papa Francis nchini Irak

Wataalamu wa afya wamemuonya Papa Francis kuahirisha ziara yake nchini Irak inayopangwa Ijumaa,kwa hofu ya kuona ongezeko la maambukizi nchini humo kutokana na mikusanyiko ya umma.

Ufilipino imeanzisha leo Juamtatu kampeni yake ya chanjo dhidi ya virusi vya Corona. Rais Rodrigo Duterte na maafisa wengine wa serikali walikuwa wakwanza kupewa chanjo hiyo.

Nigeria itakuwa nchi ya tatu barani Afrika baada ya Ghana na Ivory Coast kupokea shehena ya kwanza hapo kesho ya chanjo ya Covax. Kwa jumla Nigeria iliagiza dozi milioni 16 ya chanjo dhidi ya virusi vya Corona.