1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza na Uturuki zaungana kupambana na uhamiaji haramu

9 Agosti 2023

Uingereza imetangaza makubaliano na Uturuki ya kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na uhamiaji haramu. Mpango huo unajumuisha kituo kipya cha utendaji bora kitakachoanzishwa na jeshi la polisi la Uturuki.

https://p.dw.com/p/4UwnV
Seenotrettung Mittelmeer
Picha: Joan Mateu Parra/AP/dpa/picture alliance

London imetangaza mpango huo jana usiku kama sehemu ya jitihada zake za kupunguza uhamiaji haramu nchini Uingereza, ambao ni suala muhimu la kisiasa.

Kituo hicho kipya kitakachoungwa mkono na Uingereza kitasaidia kuimarisha utalaamu uliopo kati ya nchi hizo mbili kuhusiana na shughuli zinazolenga kuivunja mitandao ya uhalifu inayojihusisha na usafirishaji haramu wa binaadamu.

Serikali ya Uingereza iko chini ya shinikizo la kuwazuia wahamiaji wanaovuka bahari kinyume cha sheria na kuingia nchini humo.