SiasaUingereza
Uingereza yashuku kuvamiwa kwa meli mlango bahari wa Hormuz
13 Aprili 2024Matangazo
Ingawa taarifa iliyotolewa leo na jeshi hilo haikutowa undani, tukio hilo limetokea kukiwa na mvutano kati ya Iran na mataifa ya Magharibi, hasa baada ya mashambulizi yanayoshukiwa kufanywa na Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria.
Iran haikutowa taarifa ya kuishikilia meli hiyo, wala ripoti hiyo haikutangazwa kwenye vyombo vya habari vya nchi hiyo.
Mlango Bahari wa Hormuz ni ujia wa maji unaopatikana kwenye ghuba ya Uajemi ambayo inapitisha karibu asilimia 20 ya mafuta yote yanayosafirishwa duniani.
Tangu mwaka 2019 Iran imehusika kwenye matukio kadhaa ya kuzishikilia meli katika eneo hilo na kumekuwa na mashambulizi dhidi ya vyombo vya baharini yanayohusishwa na mzozo wake na mataifa ya Magharibi.