1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Uingereza yasema inaisaidia Israel kuwatafuta mateka

3 Desemba 2023

Uingereza inaiunga mkono Israel katika harakati zake za kuwatafuta mateka ambao bado wanashikiliwa na kundi la wanamgambo la Hamas katika ukanda wa Gaza. Hii ni kulingana na taarifa ya serikali ya Uingereza.

https://p.dw.com/p/4Zio4
Ujumbe wa kutaka mateka waachiliwe huru unasomeka "warejesheni nyumbani"
Inakadiriwa zaidi ya mateka 100 wa Israel bado wamo mikononi mwa kundi la Hamas. Wachache wengine waliachiwa siku za hivi karibuni.Picha: GIL COHEN-MAGEN/AFP/Getty Images

Katika tangazo lake la jana jioni, serikali hiyo imesema kuwa kwa kuunga mkono operesheni hiyo ya kuwaokoa mateka wa Israel, wizara ya ulinzi ya Uingereza itapeleka ndege zake za ufuatiliaji Mashariki mwa Mediterenia pamoja na anga ya Israel na Gaza.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa ndege hizo za ufuatiliaji hazina silaha na hutumika kutambua maeneo ya mateka na kwamba habari za pekee zinazohusiana na uokoaji wa mateka hao, zitawasilishwa kwa mamlaka husika.

Takriban watu 240 walitekwa nyara na wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas wakati wa uvamizi wa kushtukiza dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7 mwaka huu.