1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Uingereza yakanusha ripoti za kifo cha Mfalme Charles III

Hawa Bihoga
19 Machi 2024

Balozi za Uingereza mjini Moscow na Kyiv jana Jumatatu zilikanusha ripoti za vyombo vya habari vya Urusi zilizodai kuwa Mfalme Charles wa III amekufa.

https://p.dw.com/p/4dsiW
London | Mfalme wa Uingereza Charles III
Mfalme wa Uingereza Charles IIIPicha: Victoria Jones/empics/picture alliance

Ripoti hizo za uongo zilianza kusambaa Jumatatu mchana kwenye kurasa za lugha ya Kirusi kwenye mtandao, zikichochewa na chaneli za Telegram zinazojikita katika ripoti zilizotiwa chumvi. 

Familia ya Kifalme ya Uingereza hivi sasa inakabiliwa na uvumi mwingi na nadharia za njama kufuatia hali ya mfalme na mkwe wake Kate. 

Soma pia:Mfalme Charles III wa Uingereza agunduliwa na saratani

Charles anatibiwa kutoka na saratani, lakini anaendelea kusimamia masuala ya taifa. Kwa upande wake, Kate anaendelea kupona kutokana na operesheni na hatarajiwi kuonekana hadharani tena hadi baada ya Pasaka.