1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Uingereza yahofia udukuzi katika uchaguzi wake mkuu

30 Juni 2024

Naibu waziri mkuu wa Uingereza Oliver Dowden ameonya kwamba uchaguzi mkuu ujao unakabiliwa na vitisho vya nje kama vile Urusi, ambayo amesema inalenga kushawishi mchakato wa kidemokrasia wa Uingereza.

https://p.dw.com/p/4hh3j
Uingereza |
Naibu waziri mkuu wa Uingereza Oliver Dowden ahofia udukuzi katika uchaguzi wa mkuu ujao.Picha: Yui Mok/empics/picture alliance

Kauli hii inajiri baada ya Shirika la Utangazaji la Australia kuripoti kwamba limefichua kurasa tano za Facebook zinazoeneza hoja ambazo zinaungwa mkono na Kremlin.

Soma pia: Sunak na Starmer wakabiliana katika mdahalo wa mwisho kabla ya uchaguzi Uingereza

Uingereza itapiga kura siku ya Alhamisi, katika uchaguzi unaotarajiwa kukitimua chama tawala cha mrengo wa kulia cha Conservatives na kukiweka madarakani chama cha upinzani cha Labour.

Brexiteer Nigel Farage mpinzani mkuu kwa chama cha Conservatives na mfuasi wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, amekanusha madai kwamba Urusi inaweza kuingilia na kushawishi matokeo ya uchaguzi wa Uingereza.