1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yahofia mashambulizi ya kigaidi ziara ya Biden

28 Machi 2023

Serikali ya Uingereza imeongeza kiwango cha tahadhari kuhusu kitisho cha kutokea mashambulizi ya kigaidi katika jimbo la Ireland ya Kaskazini kabla ya ziara inayotarajiwa ya Rais Joe Biden wa Marekani.

https://p.dw.com/p/4POVJ
USA Nashville | Schießerei an Covenant School
Picha: Alex Brandon/AP/picture alliance

Rais huyo wa Marekani anatarajiwa kuhudhuria kumbukumbu ya miaka 25 tangu yalipofikiwa makubaliano ya amani ya kihistoria, Aprili 10 mwaka 1998 yanayotambuliwa kama "Makubaliano ya Ijumaa Kuu", ambayo yalimaliza machafuko ya umwagaji damu Ireland Kaskazini.

Kwa mujibu wa  kiongozi mkuu wa Ireland Kaskazini, Chris Heaton-Harris, Shirika la Ujasusi la Uingereza (MI5), linaamini kitisho cha kutokea mashambulizi ni kikubwa.

Ametowa mwito kwa umma wa Ireland Kaskazini kuwa makini lakini pia kutotaharuki kufuatia tangazo hilo.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW