1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Uingereza kuimarisha uwepo wa kijeshi Ulaya Kaskazini

Josephat Charo
13 Oktoba 2023

Waziri MKuu wa Uingereza Rishi Sunak amekutana na viongozi wenzake kama sehemu ya mkutano wa kilele wa kundi la ushirikiano wa pamoja wa ulinzi.

https://p.dw.com/p/4XVoy
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na mwenzie wa Italia Gergia Meloni
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na mwenzie wa Italia Gergia MeloniPicha: Simon Dawson/Photoshot/picture alliance

Uingereza imesema inapanga kuimarisha uwepo wake wa kijeshi Ulaya Kaskazini, ikiwemo kupeleka vikosi 20,000 vya wanajeshi katika eneo hilo mwaka ujao, kusaidia kuilinda miundombinu muhimu wakati wasiwasi ukiongezeka kuhusu hujuma ya Urusi.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amekutana mapema leo na viongozi wenzake kama sehemu ya mkutano wa kilele wa kundi la ushirikiano wa pamoja wa ulinzi katika kisiwa cha Scotland cha Gotland katika bahari ya Baltic.

Kundi hilo linazijumuisha nchi za Ulaya kaskazini na eneo la Baltic, Uholanzi na Uingereza. Uingereza imesema katika taarifa kwamba itatuma wanajeshi 20,000, wanamaji na wanajeshi wa anga pamoja na manuwari nane za jeshi la majini, ndege za kivita na helikopta za kijeshi kusaidia polisi na kuepusha kitisho kutoka kwa Urusi.