1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Boris Johnson aamua bunge lisitishe vikao kwa muda

28 Agosti 2019

Hatua ya Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kusababisha bunge kusitisha vikao vyake imezusha mjadala. Kiongozi wa upinzani Jeremy Corbyn akimwandikia barua Malkia Elizabeth kueleza kusikitishwa kwake na mpango huo.

https://p.dw.com/p/3OdeU
Frankreich G7 Gipfel in Biarritz | Boris Johnson
Picha: picture-alliance/dpa/M. Kapeller

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour nchini Uingereza Jeremy Corbyn amemwandikia barua Malkia Elizabeth kueleza kusikitishwa kwake na mpango wa waziri mkuu wa taifa hilo Boris Johnson wa kusitisha shughuli za bunge hadi Oktoba 14 baada ya malkia kuridhia ombi la serikali.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya chama hicho, Corbyin pia ameomba kukutana na Malkia Elizabeth. Chama kingine kidogo cha kiliberali cha upinzani, ambacho kimekuwa kikipinga hatua ya Uingereza kujiondoka katika Umoja wa Ulaya-Brexit, nacho kimeandika barua inayofanana na ya Corbyn kwa Malkia kuonesha kusikitishwa kwao na hatua ya Boris Jonhson.

Katika muendelezo wa kupingana na jitihada za Johnson, Ireland vilevile imesema haitabadili msimamo wake kuhusu hatua ya Brexit. Akiulizwa na mtangazaji wa kituo cha redio cha taifa RTE, kuhusu msimamo wa Ireland baada ya hatua ya waziri mkuu wa Uingereza, ambayo itaweza kuzuia nafasi ya bunge kuijadili Brexit kabla ya tarehe ya mwisho ya makubaliono ya mpango huo ya Oktoba 31, waziri wa upande wa Ireland,  Paschal Donohoe aliongeza kwa kusema hakuna uondokaji wa holela wa Uingereza katika Umoja usiweza kuepukika.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour nchini Uingereza Jeremy Corbyn amemwandikia barua Malkia Elizabeth kueleza kusikitishwa kwake na mpango wa waziri mkuu wa taifa hilo Boris Johnson
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour nchini Uingereza Jeremy Corbyn amemwandikia barua Malkia Elizabeth kueleza kusikitishwa kwake na mpango wa waziri mkuu wa taifa hilo Boris JohnsonPicha: picture-alliance/empics/A. Chown

Kwa upande wake Waziri wa kiongozi wa Scotland, Nicola Surgeon amesema:

"Kulifunga bunge ili kulazimisha Uingereza kuondoka katika Umoja wa Ulaya bila makubaliano jambo litakalosababisha athari kubwa na ya muda mrefu kwa taifa, kinyume na matakwa ya bunge, ni udiktekta. Na kama wabunge hawajaungana pamoja kumzuia Boris Johnson na mwenendo wake, nadhani kwa sasa demokrasia ya Uingereza utakuwa inakufa"

Mapema leo Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amefanya jaribio la kudhibiti fursa ya fursa ya bunge kujaidili mchakato wa Brexit kwa kupunguza muda kuanzia sasa hadi tarehe iliyopangwa na Umoja wa Ulaya ya taifa hilo kujiondoa ya Oktoba 31, akiwagadhibisha wapinzani wanaomtuhumu kuendesha mambo kwa kutumia mabavu.

Jitihada yake ya sasa ni kuiondoa Uingereza nje ya Umoja wa Ulaya iwe kwa makubaliano au kinyume chake. Hatua ya sasa inaweza kufanikishwa kuhitimishwa kwa ngwe ya vikao vya bunge la Uingereza katikati ya mwezi ujao ikiwa ni takribani mwezi mmoja kabla ya tarehe ya mwisho ya Brexit.

Kwa wanaopinga mpango wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya bila ya maridhiano, unapungua pia muda wa kuwasilisha mswaada wa sheria kuzuwia nchi hiyo kujitoa kwa kila hali ifikapo Oktoba 31 inayokuja.