1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUhispania

Uhispania: Maelfu waandamana kudai nuymba za bei nafuu

14 Oktoba 2024

Maelfu ya watu waliandamana mjini Madrid nchini Uhispania Jumapili, kudai nyumba za bei nafuu huku bei ya kukodisha nyumba ikipanda.

https://p.dw.com/p/4ljz3
Waandamanaji mjini  Madrid Uhispania wadai nyumba za bei nafuu katika maandamano waliofanya Oktoba 13
Waandamanaji mjini Madrid Uhispania wadai nyumba za bei nafuuPicha: Luis Soto/Zuma/picture alliance

Chini ya kauli mbiu "Nyumba ni haki, sio biashara" waandamanaji walitoa wito wa kupunguzwa kwa kodi na kuimarishwa kwa hali ya maisha.

Serikali inakadiria kuwa takriban watu 22,000 walishiriki katika maandamano hayo ijapokuwa waandaji wanadai kuwa watu wanaofikia 150,000 walishiriki.

Soma pia:Maelfu waandamana kupinga mipango ya kaimu waziri mkuu Sanchez nchini Uhispania

Mnamo mwezi Julai, serikali ya Uhispania ilitangaza msako dhidi ya nyumba za kuishi kwa muda ama pia za likizo za muda mfupi kuthibitisha kama zina leseni za kukodisha.

Katikamaandamano tofauti huko Barcelona, ​​raia tayari wamelalamika dhidi ya utalii wa kupita kiasi katika mji huo maarufu wa pwani.

Sasa wanahoji uamuzi wa mamlaka kuandaa Kombe la Amerika mwishoni mwa msimu wa kiangazi unaoshuhudia watalii wengi.