1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Suala la Uhamiaji lajadiliwa na mawaziri wa Umoja wa Ulaya

Shisia Wasilwa
12 Julai 2018

Waziri wa mambo ya ndani wa Italia Matteo Salvini ameapa kuwashtaki wahamiaji waliookolewa kwenye fukwe za Libya wiki iliyopita akiwaita kuwa ni "wahalifu".

https://p.dw.com/p/31Lbc
Österreich Innsbruck - EU-Innenminister | Seehofer, Deutschland Kickl, Österreich & Salvini, Italien
Picha: DW/B. Riegert

Haya yanakuja wakati mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya wakikutana nchini Austria kusaka mbinu za kukabiliana na tatizo la wahamiaji, kwenye majira haya ya kiangazi ambayo hutumiwa sana na wahamiaji kuingia barani Ulaya. Kwa sasa meli ya Italia inasubiri kupata idhini ya kuwaondoa wahamiaji hao, huku Ufaransa ikiwapokea wahamiaji wa Eritria na Sudan waliokataliwa kwenye bandari za Malta na Italia.

Mawaziri hao wa mataifa 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya wanakabiliwa na shinikizo za kuanzisha sera mpya kudhibiti wahamiaji wapya, huku Austria ikiapa kuchukua msimamo mkali.

Italia na Malta zakataa kuruhusu meli ya wahamiaji

Waziri wa Uchukuzi wa Italia, Danilo Toninelli, amesema baadhi ya wahamiaji hao 67 waliokataliwa wametoa vitisho vya kuwaua wafanyikazi wa meli hiyo kwa kuhofia kurejeshwa kwenye vituo ambavyo hutumika kuwazuia wahamiaji nchini Libya. Waziri wa masuala ya Ndani wa Italia, Mateo Salvini, ameuambia mkutano wa Vienna kuwa atawachukulia hatua za kisheria wahamiaji hao aliosema ni wahalifu.

Waziri wa masuala ya Ndani wa Italia Matteo Salvini
Waziri wa masuala ya Ndani wa Italia Matteo SalviniPicha: Reuters/S. Rellandini

Salvini, amesema, “nimeridhishwa na mapendekezo ya Italia ambayo huenda yakawa ya mataifa ya Ulaya. Kupunguza idadi ya wakimbizi wanaokuja ulaya, kupunguza vifo na hivyo kupunguza matatizo ya kiuchumi na gharama ya wahamiaji ambayo hatuwezi tena kumudu. Hatimaye Umoja wa Ulaya utaanza tena kuilinda mipaka yake na kulinda watu milioni 500 ambao usalama wao ulikuwa hatarini miaka ya nyuma.”

Hata hivyo, vitisho vya wahamiaji hao vimeitikiwa na serikali ya Italia kwa kuwahamishia kwenye meli moja iliyoko kwenye fukwe za Trapani nchini Italia. Kwenye fukwe hiyo waandamanaji walikuwa wakipinga msimamo mkali wa Italia kuhusu suala la wahamiaji.

Wengi walivalia mavazi ya rangi nyekundu ambayo ni ishara ya kuwakaribisha wahamiaji. Idadi kubwa ya waandamanaji hao pia wamevalisha watoto wao mavazi ya rangi hiyo ili kurahisisha kutambuliwa kwao iwapo mawimbi makali yanaweza kuharibu meli hiyo.

Ufaransa yawachukua wakimbizi 78 

Wahamiaji waokolewa kwenye fukwe za Libya
Wahamiaji waokolewa kwenye fukwe za Libya Picha: picture-alliance/AP/Mission Lifeline/H. Poschmann

Wakati hayo yakifanyika Ufaransa imechukua kikundi cha watu 78 wanaotafuta hifadhi. Ripoti zinasema kuwa wengi wao wanatokea mataifa ya Eritrea na Sudan baada ya mashua yao kuzuliwa kuingia katika bandari za  Italia na Malta.

Waziri wa masuala ya Ndani wa Ufaransa alisema kikundi cha wakimbizi hao kilifika nchini humo siku ya Alhamisi kutoka Uhispania baada ya meli iliyowaokoa kuruhusiwa kutia nanga mwezi uliopita.

Wizara hiyo imesema kuwa imewatambua wahamiaji hao 78 kuwa wanahitaji ulinzi kama wakimbizi na watapewa makazi katika majimbo ya Kusini mashariki na Kaskazini mwa Ufaransa.

Meli iliyokuwa inawabeba wahamiaji 630 ilivutia macho ya ulimwengu baada ya Italia na Malta kukataa kuipa ruhusu ya kutia nganga kwenye bandari zao. Ufaransa imechukua idadi ndogo ya wahamiaji katika miaka ya hivi karibuni ikilinganishwa na Ujerumani au Italia.

Mkutano wa Innsbruck utalenga hasa kuunda mpango mmoja wa uhamiaji utakaokubaliwa na mataifa wote  wanachama wa Umoja wa Ulaya, huku Austria ikilinga kubadilisha sera ya uhamiaji ya Umoja huo, ili kufanya iwe vigumu kwa wanaomba hifadhi katika mataifa ya Ulaya.

Mkutano walenga kubadilisha sera za Umoja wa Ulaya

Wahamiaji wanaomba msaada kwenye fukwe za Libya
Wahamiaji wanaomba msaada kwenye fukwe za Libya Picha: picture-alliance/dpa/O.Calvo

Waziri wa masuala ya ndani wa Austria mwenye msimamo mkali Herbert Kickl, wa chama cha mrengo wa kulia wa FPOE aliwaambia wanahabari mapema juma hili kuwa atapendekeza kuwepo kwa kambi za wakimbizo nje ya ulaya kwa wahamiaji wanaotafuta hifadhi.

Wahamiaji pekee watakaoruhusiwa kufanya maombi yao katika mataifa ya Ulaya ni wale ambao mataifa yao yanapaka na mataifa ya Umoja wa Ulaya.

Kickl anatarajiwa kushirikiana na mwenzake wa Italia Matteo Salvini, kushinikiza mapendekezo hayo.

Salvini amepiga marufuku maboti yanayomilikwa na asasi za kiraia ambazo huwachukua wahamiaji kutoka bahari ya Mediterranea kutotia nanga nchini Italia, akiwashutumu kwa kuwasaidia waluanguaji binadamu kufika Ulaya.

Mwandishi: Shisia Wasilwa, Ap, Dpa, Afp

Mhariri: Mohammed Khelef