1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUlaya

Ugiriki yashutumiwa kushindwa kusimamia mkasa wa wahamiaji

14 Desemba 2023

Makundi ya haki yasema mamlaka za Ugiriki zimeshindwa kuchunguza kikamilifu madai kwamba zilishindwa kusimamia vyema mkasa wa wahamiaji

https://p.dw.com/p/4a8jN
Haki za Binadamu | Mwanamke akitazama kibao cha Human Rights Watch
Shirika la kimataia la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch Picha: John MacDougall/AFP/Getty Images

Mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu, Amnesty International na Human Rights Watch leo yameshtumu mamlaka za Ugiriki kwa kushindwa kuchunguza ipasavyo kilichasababisha kuzama kwa boti la wahamiaji miezi sita iliyopita ambapo mamia ya watu walifariki dunia.

Katika taarifa ya pamoja, mashirika hayo yamesema kuwa ni hatua chache zilizochukuliwa katika kuchunguza madaiya baadhi ya manusura kwamba shughuli ya uokoaji ilicheleweshwa na kusimamiwa vibaya.

Soma pia:Mabaharia 12 haijulikani waliko mkasa wa kuzama meli Ugiriki

Judith Sunderland, mkurugenzi mshirika wa Human Rights Watch kwa Ulaya na Asia ya kati, ameliambia shirika la habari la AP kwamba manusura, familia za waliopotea na waliokufa, zinastahili maelezo kamili kuhusu kilichotokea.

Sunderland amesema kuwa utafiti wao umethibitisha kwamba saa chachekabla ya boti hiyo kuzama, ilionekana wazi kuwa imejaa kupita kiasi na kutokuwa salama kusafirisha abiria.

Hakukuwa na majibu ya haraka kutoka kwa mamlaka za Ugiriki kuhusiana na ripoti hiyo, lakini serikali imewatetea walinzi wa Pwani na kusisitiza kwamba wasafirishaji haramu wa watu ndio wanaopaswa kulaumiwa.