1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UGIRIKI NDIO MABINGWA WAPYA WA KOMBE LA ULAYA.WALIILAZA JANA URENO 2:1

Ramadhan Ali5 Julai 2004
https://p.dw.com/p/CHaD

MICHEZO 05-07-04

UGIRIKI NI MABINGWA WAPYA WA ULAYA NA NANI ALIETARAJIA ?

-KOCHA WA UGIRIKI OTTO REHAGHEL ATARIDHIA SASA KUWA KOCHA WA UJERUMANI ?

SIMBA WA NYIKA –KAMERUN WANGURUMA MBELE YA TEMBO WA I.COAST KATIKA KUANIA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA

Michezo ya Olimpik inaanza mjini Athens,ugiriki weiki 6 kutoka leo,lakini wanadinga wa Ugiriki wameshaparamia kilele cha mlima wao maarufu wa Olimpik: Mount Olympius. Ugiriki iliizaba jana Ureno bao 1:0 na kutoroka na Kombe hilo hadi Athens, kuanuzisha shamra shamra za michezo ya olimpik kabla ufunguzi rasmi,August 13.

Tangu msangao wa Czechoslovakia katika kombe la Ulaya la 1976 mjini Belgrade na Denmark, 1992 ,zilipoilaza Ujerumanio na kutoroka na Kombe hili la Ulaya, huu ni msangao 3 katika historia ya miaka 40 ya Kombe hili.Kwani, wiki tatu tu nyuma Ugiriki ikihesabiwa kuwa mojawapo ya timu zilizoshindwa kufua dafu kwa kushinda alao mpambano mmoja katika mashindano makuu kama haya au Kombe la dunia.Jana,lakini walivunja mwiko huo na wao na sio,Ufaransa,Ujerumani,Itali,Uingereza,Spain au wenyeji Ureno waliotawazwa mabingwa wa Kombe la Ulaya.

Bao la Ugiriki lililitiwa na HARISTEAS mnamo dakika ya 57 ya mchezo.Haristeas anaichezea Weder Bremen,klabu bingwa ya Ujerumani ambako kocha wao Ugiriki Otto Rehagel,alikuwa mwalimu miaka kadhaa na kuitawaza klabub hiyo mabingwa.

Ugiriki inayoomboleza hjadi leo kwa kulikosa Kombe iliingia jana finali yake ya kwanza ya mashindanomakuu.Ilifaidika kama Ugiriki na ustadi wa kocha wao wa kigeni-mbrazil Felipe Scolari na nafuu kwamba wakicheza nyumbani.

Sekunde tu firimbi ya mwisho kulia jana kengele za makanisani zilihanikiza nchini kote Ugiriki n a magari yakipiga honi katika majia ya miji mikuu ya ureno.Kila upitapo hali ilikua hiyo hiyo,bahari ya bendera za bluu na nyeupe,ilikua hivyo mjini Athens,ugiriki,mjini Lisbon,Ureno,mtaa wa wagiriki mjini London na New York.Fashi-fashi ziligeuza baadhi ya mitaa kuwa kama kumeripuka vita kwa mishindo ya mizinga.sababu ya yote hayo ni shetani wa mpira aliepungwa sio tu Ulaya bali hata Afrika na Asia.Nchini Indonesia watu waliahirisha kwenda kupiga kura leo,kwavile wakikodoa macho usiku mzima kuangalia finali ya Kombe la Ulya-la pili kwa ukali na msisimko baaada ya Kombe la dunia la FIFA.

Haya ni makaribisho makubwa kwa michezo ijayo ya olimpik mwezi ujao.Kwani, yanawafanya wagiriki kusahau taabu na shida na gharama za kuandaa michezo kama hiyo .Wanaelewa mhanga wanaobidi kuutoa kwa michezo inayorudi nyumbani kama timu yao hii leo.

Ugiriki ndio imetawazwa mabingwa wa Ulaya,lakini mbinu za mchezo alizotumia kocha wao-mjerumani Otto rehagel zilifaa ? je, muhimu leo ni ushindi tu bila kujali mchezo wenyewe unavyostarehesha mashabiki ? Na je, Otto Rehagel baada ya kitawaza Ugiriki mabingwa wa Ulaya jana,atakubali kuiachamkono sasa Ugiriki na kuwa kocha wa Timu ya taifa ya Ujerumani inayosaka wa kuongoza wakati huu.

Shirikisho la dimba la Ujerumani DFB lakutana hii leo mjini Frankfurt na Otto bila shaka anazungumzwa na miujiza yake ya dimba alioionesha huko Lisbon:

Makocha kadhaa wamefyekwa au wamejiuzulu kufuatia kupigwa kumbo kwa timu zao na mapema katika Kombe hili la Ulaya:Wakwanza alikua kocha wa Ujerumani-Rudi Völler,baadae wa Spain na hata wa Itali giovanni Trapattoni.Trapattoni ameshatangazwa leo atakua kocha wa Benefica Lisbon,klabu ya ureno.kocha wa hadi sasa wa Benefica Lisbon-klabu ya mwanamsumbiji Eusebio, Jose Antonio Camacho aliachamkono hapo Mei mwaka huu ili kuwa kocha wa Real Madrid ya spain.

MWISHOE: KANDA YA AFRIKA NA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA 2006 UJERUMANI:

Katika changamoto za jana za kuania tiketi za Kombe hilo la dunia, Simba wa nyika Cameroun,ilinguruma mara 2 mnamo dakika 3 za kuilaza Ivory Coast kwa mabao 2:0 na hivyo kuliacha kundi hili wazi kuhusu nani angekata tiketi ya kombe la dunia.Kushindwa kwa Cameroun jana kungewaacha pointi 5 nyuma ya Tembo wa Ivory Coast na ndoto yao yakuja Ujerumani kwa Kombe la dunia na kwa mara ya 5 kucheza katika Ko mbe hilo ingeshindwa kutimilia.Mchezaji bora wa mwaka wa dimba wa Afrika Samuel Eto’o alitikisa wavu mnamo dakika ya 80 ya mchezo na mbele ya mashabiki wa nyumbani 75.000 katika uwanja wa Ahmadou Ahidjou,mjini Yaounde.Guy Feutchine aliekuja uwanjani baadae,akamaliza udhia kwa bao la pili la Cameroun.

Mpambano mwengine wa kundi hili la 3 ulimalizika pia kwa msangao pale Benin ilipozima vishindo vya mafirauni wa Misri kwa kuachana nao sare 3:3 mjini Cotonou.

Huku Libya ikiwa imeondoka kwa msangao na ushindi wa bao 1:0 dhidi ya Sudan hapo jumamosi,ni mwanya wa pointi 3 unaozitenganisha timu 4 za usoni.Cameroun ina pointi 7,I.Coast pointi 6 huku Misri na Libya kila moja ikiwa na pointi 4-Mapambano 7 yamesalia kabla kutia tiketi mfukoni kuja Ujerumani 2006.

Congo iko mbele ya Senegal kwa tofauti ya magoli.Togo,Zambia na Liberia kila moja ina pointi 4 katika kundi lao.