1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yapuuza upelelezi kuhusu Bobi Wine

30 Agosti 2018

Msemaji wa serikali ya Uganda ameutupilia mbali wito wa Umoja Mataifa kutaka uchunguzi huru kutokana na machafuko baada ya kukamatwa na kuteswa kwa wabunge kadhaa, akiwemo nyota wa muziki Bobi Wine.

https://p.dw.com/p/343hO
Maanamano kumuunga mkono Bobi Wine | ARCHIV
Picha: Getty Images/AFP/I. Kasamani

J3 30.08Uganda: independent investigation on Bobi Wine - MP3-Stereo

Serikali imesema kuwa polisi ya Uganda pamoja na vyombo vingine vya usalama vina uwezo wa kuendesha uchunguzi huo. Kauli hii ya Opondo inatokana na msimamo wa mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Al Hussein, aliyetolea wito serikali ya Rais Yoweri Museveni kuhakikisha unafanyika uchunguzi huru juu ya ghasia hizo, yakiwemo madai ya mauaji ya makusudi, matumizi ya nguvu kupita kiasi na mateso yaliyofanywa na polisi. Mwandishi wetu Lubega Emmanuel ametutumia ripoti hii.