1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Uganda yamkamata mshukiwa wa mkanyagano wa mwaka mpya

9 Januari 2023

Polisi ya Uganda leo imesema imemkamata mshukiwa mkuu aliyetoroka baada ya mkanyagano uliosababisha vifo katika hafla moja ya mkesha wa Mwaka Mpya.

https://p.dw.com/p/4LvFY
Uganda Kampala Silvester Feuerwerk
Picha: Badru Katumba/AFP/Getty Images

Polisi ya Uganda leo imesema imemkamata mshukiwa mkuu aliyetoroka baada ya mkanyagano uliosababisha vifo katika hafla moja ya mkesha wa Mwaka Mpya. Msemaji wa polisi ya Kampala Patrick Onyango ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba, Elvis Francis Juuko alikamatwa Ijumaa iliyopita alikokuwa amejificha huko Mityana, karibu kilomita 60 magharibi mwa Kampala. Onyango lakini hakusema ni lini mshukiwa huyo atafikishwa mahakamani. Polisi inamtuhumu Juuko kwa kuwashawishi watu waliokuwa katika hafla hiyo kupitia njia nyembamba kutazama fataki, jambo lililochochea mkanyagano huo. Watu kumi wengi wao wakiwa watoto waliuwawa katika mkanyagano huo.