1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda kuwaondoa wanajeshi wake Mashariki mwa Congo

17 Mei 2022

Uganda imesema itawaondoa wanajeshi wake kutoka mashariki mwa Jamhri ya Kidemokrasi ya Congo katika wiki mbili zijazo. Kamanda wa jeshi la ardhini la Uganda amesema wanajeshi hao wataondolewa huko wiki mbili zijazo.

https://p.dw.com/p/4BQKX
Uganda UPDF Truppen Armee
Picha: Getty Images/AFP/P. Busomoke

Kamanda wa jeshi la ardhini la Uganda Muhozi Kainerugaba amesema Operation Shujaa ambayo ilitakiwa kudumu kwa miezi sita, itafikia kikomo rasmi takriban wiki mbili zijazo. 

Muhozi ambaye ni mtoto wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema kama hatapata maelekezo zaidi kutoka kwa kamanda mkuu wa majeshi ya Uganda au mnadhimu wa jeshi, basi atawaondoa wanajeshi wote. 

Serikali ya Uganda iliwapeleka mamia ya wanajeshi mashariki mwa Congo mwezi Desemba mwaka uliopita kulisaidia jeshi la Congo kuzishambulia kambi za kundi la waasi wa Allied Democratic Forces ADF.

Hakuna sababu zozote zilizotolewa kwa mpango wa kuwaondoa wanajeshi hao wala taarifa mpya kuhusu operesheni dhidi ya ADF.

Chanzo: afp