1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaUganda

Uganda kuharibu dozi za chanjo ya uviko-19

11 Januari 2024

Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali nchini Uganda, amesema nchi hiyo itaharibu chanjo za Uviko-19 zilizovuka muda wake wa matumizi zenye thamani ya dola milioni 7.4, kufuatia kupungua kwa mahitaji ya chanjo hizo.

https://p.dw.com/p/4b7BR
Uganda yaharibu chanjo ya uviko-19
Uganda yaharibu chanjo ya uviko-19Picha: Sovannara/Xinhua/IMAGO

Uganda ilitumia mkopo kutoka Benki ya Dunia kuagiza chanjo hizo, na takribani nusu ya shehena ya dozi milioni 12.6 zimeisha muda wake, kulinga na ripoti iliyotolewa na mkaguzi mkuu kwa bunge la Uganda. Shehena zaidi ya chanjo inatazamiwa pia kuisha muda wake wa matumizi ifikapo mwishoni mwa mwaka mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari ya taifa ya dawa, inayosambaza dawa kwa vituo vya afya nchini humo, Moses Kamabare, alisema mamlaka itaanza kuharibu chanjo zilizoisha muda wake haraka iwezekanavyo.

Waziri wa afya wa Uganda Ruth Aceng, aliliambia bunge mnamo Oktoba mwaka jana, kwamba karibu asilimia 59 ya Waganda walipata chanjo kamili dhidi ya Uviko-19.