1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki Paris 2024

27 Julai 2024

Shamrashamra za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 zilishuhudiwa Ijuma usiku katika mto Seine.

https://p.dw.com/p/4iotE
Mchezaji nyota wa zamani wa Ufaransa Zinedine Zidane
Mchezaji nyota wa zamani wa Ufaransa Zinedine Zidane Picha: LOIC VENANCE/Pool via REUTERS

Miongoni mwa mambo mengine kulikuwepo burudani ya muziki kutoka kwa wasanii maarufu duniani kama Celine Dion, Lady Gaga na Aya Nakamura.

Usalama uliimarishwa ambapo polisi na wanajeshi wapatao 45,000 walisambazwa sehemu mbalimbali. Zaidi ya wakuu 100 wa nchi walihudhuria hafla hiyo ya ufunguzi akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mke wa Rais wa Marekani Jill Biden miongoni mwa viongozi wengine.

Soma zaidi: Paris yanga'a katika sherehe ya ufunguzi ya michezo ya Olimpiki

Hayo yakiarifiwa, usafiri wa treni za mwendo kasi nchini Ufaransa umerejea hivi leo katika hali ya kawaida baada ya wahandisi kufanya kazi usiku kucha kukarabati vituo na nyaya zilizoharibiwa katika kile maafisa walisema ilikuwa vitendo vya hujuma.