1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfilipino

Marekani na Ufilipino waungana dhidi ya uchokozi wa China

2 Mei 2023

Rais wa Marekani amemwambia mwenzake wa Ufilipino kuwa ahadi ya nchi yake juu ya ulinzi wa mshirika wake huyo, ni thabiti ikiwemo eneo la Bahari ya Kusini mwa China ambako Ufilipino inapitia shinikizo kubwa kutoka China.

https://p.dw.com/p/4QnFE
USA Biden empfängt den philippinischen Präsidenten im Weißen Haus
Picha: Carolyn Kaster/AP/dpa/picture alliance

Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr. ambaye yupo katika ziara yake ya kwanza ya Ikulu ya Marekani kuwahi kufanywa na kiongozi wa Ufilipino katika miaka 10 iliyopita, alisisitiza umuhimu wa Marekani kuwa mshirika wa kipekee wa nchi yake katika kanda hiyo ambayo kwa sasa inapitia hali ngumu ya kisiasa duniani.

Mataifa hayo mawili Marekani na Ufilipino, yalihakikishiana tena ushirikiano wao wa ulinzi, katika ziara ambayo ilibadilisha mkondo mzima wa uhusiano wa mataifa hayo ambayo yote mawili yanatafuta njia za kuidhibiti China, wanayosema inazidisha hatua zake za kichokozi karibu na Taiwan na katika bahari ya Kusini mwa China.

Umoja wa UIaya wataka ulinzi katika Ujia wa Taiwan

Maafisa wa Marekani wamesema viongozi hao Rais Joe Biden wa Marekani na Marcos Jr wa Ufilipino, watakubaliana kuhusu miongozo mipya ya ushirikiano imara zaidi wa kijeshi pamoja na kiuchumi.

Baada ya Joe Biden kutoa tamko lake la kuimarisha zaidi mahusiano yao, taarifa ya pamoja ilisema kuwa hii inamaanisha kwamba, shambulio lolote dhidi ya jeshi la Ufilipino, meli zake, au ndege zake katika eneo la pasifiki, ikiwemo Kusini mwa bahari ya China, itapelekea Marekani kuilinda Ufilipino chini ya mkataba wa ulinzi uliotiwa saini mwaka 1951.

Marekani inaiona Ufilipino kama mshirika muhimu wa kuzuwia uvamizi wa aina yoyote utakaofanywa na China katika kisiwa cha Taiwan. China inaamini kisiwa hicho kinachojitawala chenyewe ni sehemu ya dola lake. Hivi karibuni Ufilipino iliridhia Marekani kufikia makambi yake mengine manne ya kijeshi chini ya makubaliano ya ulinzi. Lakini pande zote mbili bado hazijatangaza ni vifaa vya aina gani vya kijeshi vitakavyowekwa huko na Marekani.

Biden na Marcos Jr wakubaliana kuhusu umuhimu wa amani ya Taiwan

USA Biden empfängt den philippinischen Präsidenten im Weißen Haus
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na mwenzake wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr katika Ikulu ya MarekaniPicha: Brendan Smialowski/Pool via AP/picture alliance

Viongozi hao wawili pia wamekubaliana kuhusu umuhimu wa kuzingatia au kuhakikisha amani na udhabiti katika maeneo yanayokizunguka kisiwa cha Taiwan. Hata hivyo chini ya uongozi wa  Rodrigo Duterte, ambaye ni mtangulizi wa Marcos, mahusiano ya Marekani na Ufilipino yaliingia doa baada ya rais huyo wa zamani kujenga mahusiano ya karibu zaidi na China.

Uhusiano wa Ulaya na China kupimwa kutokana na tabia za China

Katika ziara hiyo rais Ferdinand Marcos Jr, amesema ni muhimu kwa nchi yake kuwa na mahusiano imara na mshirika wake ambaye ni Marekani, kuyafufua tena mahusiano yao hasa wakati huu ambako kuna kitisho na wasiwasi unaoonekana katika eneo la Kusini mwa China, eneo la Pasifiki na indo pasifik.

Marcos yuko katika ziara ya siku nne nchini Marekani iliyoanza siku ya Jumapili.

Alipokuwa njiani akielekea Marekani rais huyo wa Ufilipino aliwaambia waandishi habari kuwa China ilikubali kujadili haki ya uvuvi katika bahari ya Kusini mwa china na pia kwamba hatokubali Ufilipino kutumiwa kama eneo la kushambulia kijeshi.

Chanzo: Reuters