1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yatilia mashaka mazungumzo ya nyuklia ya Iran

8 Desemba 2021

Afisa wa Umoja wa Ulaya anayesimamia mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na Mataifa yalio na nguvu duniani Enrique Mora, amesema mazungumzo hayo yanayolenga kuufufua mkataba wa nyuklia ya Iran yataanza kesho Vienna.

https://p.dw.com/p/440B7
Frankreich | Minister Jean-Yves Le Drian
Picha: imago images/IP3press/V. Isore

Enrique Mora ameandika katika mtandao wake wa twitter kwamba pande husika katika mkataba wa nyuklia uliotiwa saini mwaka 2015, zitakutana katika mji mkuu wa Austria Vienna baada ya majadiliano na serikali zao yaliofanyika hivi karibuni.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean Yves Le Drian amesema pia kuwa huenda mazungumzo yakaendelea kesho huku akiitilia mashaka Iran akisema inacheza na muda.

Kwa upande wake muakilishi wa ngazi za juu wa Urusi ameelezea matumaini ya kufikiwa makubaliano mapya katika mazungumzo hayo. Mikhail Ulyanov ameandika katika mtandao wake wa twitter kwamba kushiriki kwa pande zote mbili, Marekani na Iran kunaonesha nia yao ya kweli kuelekea kuufufua mkataba huo licha ya misimamo yao kuwa tofauti. Amesema kazi ya wapatanishi ni kuondoa tofauti hizo ili kuelekea katika Umoja.

Joe Biden asema Marekani iko tayari kurejea katika mkataba wa nyuklia

USA COVID-19 | PK Biden zu Omikron
Rais wa Marekani Joe Biden Picha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Awali wanadiplomasia wa Ulaya walitoa wito kwa Iran kurejea katika majadiliano hayo yanayolenga kuufufua mkataba juu ya mpango wake wa nyuklia na mapendekezo yanayoeleweka na yanayofaa.

Wiki iliyopita Iran kuja na masharti magumu yaliotajwa kama yasiokubalika na upande wa pili katika majadiliano hayo ambao ni Uingereza, China, Ufaransa Ujerumani na Urusi.

Marekani ilijiondoa katika mkataba huo mwaka 2018 chini ya rais wa zamani Donald Trump na kurejesha vikwazo dhidi ya Iran. Hata hivyo Rais wa sasa Joe Biden amesema Marekani iko tayari kujiunga tena na mkataba huo unaonuiwa kuizuwiya Iran kuendelea na mpango wako wa nyuklia ili iondolewe vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa.

Baada ya kurudishiwa  vikwazo  na utawala wa Trump, Iran ilijibu kwa kukiuka viwango vya urutubishaji wa madini ya urani vilivyokuwa vimewekwa chini ya makubaliano ya mwaka 2015. Pia iliwazuwiya waangalizi wa Umoja wa Mataifa wa shirika la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyukilia kufikia vinu vyake hali inayozidisha wasiwasi kuhus kile Iran inachokifanya.

Maafisa zaidi wa Iran wawekewa vikwazo kwa kukiuka haki za binaadamu

Österreich Gebäude des Hauptsitzes der Internationalen Atomenergie-Organisation (IAEA)
Bebdera ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran ikionekana nje ya jengo la shirika la kudhibiti matumizi ya nishati za nyuklia IAEAPicha: Michael Gruber/Getty Images

Huku hayo yakiarifiwa Marekani imewaekea vikwazo vipya maafisa wa Iran pamoja na taasisi kadhaa kwa tuhuma za ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu siku moja kabla ya kuanza kwa mazungumzo ya vienna.

Israel yataka Iran isilegezewe masharti kuhusu nyuklia

Vikwazo hivyo vilivyotangazwa kwa ushirikiano wa wizara ya fedha na ile ya mambo ya nje viliwalenga maafisa wa serikali na mashirika yaliohusishwa na ukandamizaji wa waandamanaji na wanaharakati wa kisiasa wanaozuiliwa magerezani katika mazingira yanayoelezwa kuwa mabaya.

Chanzo: afp/ap