1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Ufaransa yapeleka wanajeshi New Caledonia kuzima ghasia

16 Mei 2024

Ufaransa imepeleka wanajeshi kwenye bandari na uwanja wa ndege wa kisiwa cha bahari ya Pasifiki kilicho chini ya milki ya Ufaransa cha New Caledonia, kupiga marufuku TikTok na kutangaza hali ya hatari.

https://p.dw.com/p/4futE
New Caledonia
Ghasia za New CaledoniaPicha: Yoan Fleurot via REUTERS

Ufaransa imepeleka wanajeshi kwenye bandari na uwanja wa ndege wa kisiwa cha bahari ya Pasifiki kilicho chini ya milki ya Ufaransa cha New Caledonia, kupiga marufuku TikTok na kutangaza hali ya hatarikufuatia machafuko ya siku tatu  ambayo yamesababisha vifo vya watu wanne na mamia kujeruhiwa.

Ghasia hizo zimechochewa na mageuzi ya katiba yanayoshinikizwa na Ufaransa kwenye kisiwa hicho kinachoendesha harakati za kutaka kujitenga.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Darmanin aliishutumu Azerbaijan kwa "kuingilia" siasa za kisiwa hicho cha New Caledonia.

Kulingana na taarifa ya ubalozi, vikosi vya usalama vya Ufaransa vimewaweka washukiwa watano ambao wanaogoza harakati hizo chini ya kizuizi cha nyumbani.

Kwa mujibu wa maafisa wa kisiwa hicho mamia ya watu, ikiwa ni pamoja na polisi 64, wamejeruhiwa, kati ya wakazi wa karibu 270,000 wa eneo hilo.

Maandamano na vurugu vyaendelea New Caledonia

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametaka mazungumzo leo Alhamisi na wabunge wa New Caledonia na kutoa wito wa kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya kisiasa.

Maandamano ya kudai uhuru, yanayoongozwa na wazawa dhidi ya mpango wa Ufaransa wa kuweka sheria mpya za upigaji kura kwenye visiwa vyake vya Pasifiki yameingia katika ghasia mbaya zaidi tangu miaka ya 1980.