1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUfaransa

Ufaransa yaisambaratisha Uholanzi 4-0

25 Machi 2023

Kylian Mbappe ameanza vyema kukitetea cheo chake cha unahodha katika timu ya taifa ya soka ya Ufaransa baada ya jana usiku kuwacharaza Uholanzi mabao 4-0.

https://p.dw.com/p/4PEUh
FIFA Fußball WM 2022 in Katar | Finale Argentinien - Frankreich
Picha: Juan Luis Diaz/Agencia MexSport/IMAGO

Na katika michezo Kylian Mbappe ameanza vyema kukitetea cheo chake cha unahodha katika timu ya taifa ya soka ya Ufaransa baada ya jana usiku kuwacharaza Uholanzi mabao 4-0 kwenye mechi ya kufuzu kushiriki michuano ya Euro 2024, huku Romelo Lukaku wa Ubelgiji akifanikiwa kuchana nyavu kwa Hat-Trick dhidi ya Sweden.

Hii ni mara ya kwanza kwa Uholanzi kufungwa mabao manne tangu ilipofungwa idadi kama hiyo na Ufaransa, mwaka 2017 mjini Paris. Katika mechi inayofuata, Ufaransa itakuwa ugenini ikikwaana na Jamhuri ya Ireland na Uholanzi ikiikaribisha Gibratal.